×

Shigongo Apokea Kilio cha Kinamama Wauza Viazi Bukokwa

MGOMBEA ubunge Jimbo la Buchosa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, leo Alhamisi, Oktoba 8, 2020 amewatembelea na kuzungumza na wafanyabiashara wadogo wa viazi vitamu katika Soko la Bukokwa Halmashauri ya Buchosa.

Akizungumza na wafanyabiashara hao ambao ni kinamama.  wamemweleza  kuwa soko hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa choo, mazingira  mabaya ya soko hilo na kumuomba endapo atachaguliwa, basi awasaidie kuboresha mazingira ya soko hilo pamoja na kuwapatia mitaji wajasiriamali hao ili waendeshe biashara yao  kwa mafanikio na hatimaye kujikwamua.

Aidha wamesema wanamuunga mkono Shigongo na kumhakikishia kwamba watampigia kura za kutosha ili akawe kipaza-sauti chao bungeni  kwani wanaamini ndiye kiongozi bora atakayewasaidia kuwaletea maendeleo na kuijenga Buchosa mpya.

 

Shigongo anaendelea na kampeni zake jimboni Buchosa akinadi sera za chama chake cha CCM  na kuwaomba ridhaa wananchi ili wawachague viongozi wa CCM kuanzia kiti cha urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

 

Leave a Comment