Macha aliandika namna hii:-“Binafsi navutiwa sana na utendaji na uchapakazi wa ndugu @antonionugaz ..Alianza kazi katika mazingira magumu sana pale Yanga. Hakuwa akifahamu mambo mengi ya soka. Ila hakukata tamaa.
“Kwanza anajiamini sana.. Very confident.(Mwenye kujiamini). Hata kama hajui kitu atapambana mpaka akifahamu. Ni watu wachache sana wenye moyo kama wake.
“Pili, yuko smart muda wote. Yaani kwa kifupi anajua kupendeza. Pengine ndiye Afisa Habari anayevaa Smart zaidi nchini. Mwonekano wake, unaakisi ukubwa wa Brand ya Yanga.
.
“Mwisho wa yote, @antonionugaz ameichangamsha sana Yanga. Amewafanya mashabiki kurejesha hali ya kujiamini na kujaa uwanjani katika mechi za Yanga. Inafurahisha sana.
“Mwisho lakini siyo wa yote. nimefuatilia Ukurasa wake hapa Instagram. Amejitofautisha sana na wengine.. Ameipa Yanga kipaumbele kuliko kitu kingine chochote. Nugaz anatumia muda wake wote kuisifia Yanga. Hana habari na Simba.
“Hapotezi muda wake kuisema vibaya Simba wala Azam. Amechagua zaidi kuisifia Yanga. Hivi ndivyo Afisa Habari anapaswa kuwa. Hatumii muda wake kutengeneza chuki kutoka timu pinzani, ila kutengeneza upendo kwa mashabiki wa Yanga kwa timu yao.
“Natumia fursa hii kumpongeza Nugaz kwa kazi nzuri. Naamini huu ni mwanzo tu, mengi mazuri yanakuja mbeleni.”

