MHARIRIMtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Saleh Ally ‘Saleh Jembe’ ametamba kuwa vijana wake wataibuka na ushindi mnono dhidi ya Azam Media FC katika mchezo mkali wa kirafi ki utakaopigwa leo Jumamosi, Dar, Uwanja wa Karume.Saleh, mshambuliaji wa kutegemewa amesema:
“Mimi nitakuwepo kwenye benchi la ufundi kesho (leo) kwani nimecheza mechi nyingi kwa hiyo nimeamua kukaa kwenye benchi kwa heshima ili kuwashuhudia vijana wangu wakiwanyoosha Azam Media,” alisema Saleh.
Alwatan Ngoda mchezaji wa Azam Media ameliambia Championi Jumamosi kuwa maandalizi yao yapo vizuri na wataingia uwanjani kwa heshima kusaka ushindi kwenye mchezo huo.
Leen Essau Dar es Salaam
