×

Mrembo Amfungia Safari Harmonize Kutoka Mara Mpaka Dar

MWANADADA, Victoria Romanus, amesafiri kutoka mkoani Mara mpaka jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuomba kazi ya unenguaji kwa msanii Rajabu Abdul ‘Harmonize’.

 

Victoria amesema yeye ni mgeni Dar es Salaam na amefikia Mbagala Mission kwa shangazi yake na kwamba anafanya kazi ya kuzunguka kwenye vyombo vya habari ili kupata msaada wa kuonana na Harmonize.

 

“Mimi nina kipaji cha sanaa ya uchezaji, nimetoka Musoma kuja Dar kwa dhumuni moja tu la kumtafuta Harmonize kwa sababu napenda kuwa mchezaji wake. Nilihangaika sana kutafuta nauli ya kuja Dar, mama yangu alikuwa hana uwezo wa kunipa nauli, hivyo nikawa natunza pesa zangu mwenyewe huku nikifanya shughuli ndogondogo kwa mwezi mmoja ili nipate nauli ya kuja huku kumpata Harmonize,” ameeleza.

 

Dada huyo hakuishia hapo kwani amefikia hatua ya kumwaga machozi kwa uchungu huku akisema anampenda sana Harmonize kuliko wasanii wote pia ndiyo shabiki yake mkubwa japo anakatishwa tamaa na watu kwamba hawezi kumpata msanii huyo.

Leave a Comment