Ni wazi hichi ni kipindi cha kufanikiwa kwenye uchumi wa utandawazi, kuanzia migahawa, magari, viwanda vidogo na vikubwa na biashara nyingine nyingi zimekuwa zikipambana zaidi kutengeneza jina kubwa kote duniani huku pia ikiangalia zaidi masoko ya ndani.
Ulimwengu wa biashara umeorodhesha kanuni hii kama “Glocalization”, Neno hili hutumiwa kuelezea bidhaa au huduma ambayo imeendelezwa na kusambazwa ulimwenguni kote lakini pia inarekebishwa ili kuendana na mahitaji ya mtumiaji katika soko la ndani.
Kiasi cha watubilioni 7.8 duniani kote wanatofautiana sana kwa upande wa mahitaji, manunuzi, mitazamo, kufikia miundombinu, umeme na mitandao ya mawasiliano.
Uwezo wa kutambua na kutengeneza bidhaa zinazokidhi mazingira tofauti ya
Watumiaji kwenye nchi tofauti na mabara imewezesha TECNO kuuza kwa kiasi kikubwa cha bidhaa bora za simu kwenye soko la Afrika, kusini na kusini mwa Bara la Asia.
UIMARA KATIKA SOKO LA SIMU
Glocalization imewezesha TECNO kujiweka kwenye nafasi ya juu kwakuwa na bidhaa bora za simu za kiganjani na kuuza bidhaa nyingi barani Afrika.
Mwezi Juni mwaka huu, TECNO ilishika nafasi ya tano kwakuwa moja ya bidhaa zinazopendwa zaidi barani Afrika.
Katika robo ya kwanza ya mwaka 2020, TECNO iliendelea kuwa na soko linalokuwa wakati duniani kote usafirishaji wa simu za kiganjani ulishuka kwa asilimia 13 kutoka mwanzoni mwa mwaka huu kwasababu ya ugonjwa wa Corona.
Katika kipindi ambacho uuzaji wa bidhaa nyingi ulishuka kwa kiwango cha tarakimu mbili, mkakati wa TECNO katika kutumia teknolojia ya kisasa kuendana na soko ulizidi kuimarika ili kuendelea kuuza simu nyingi zaidi za kiganjani kama ilivyokuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2019.
TECNO pia inafanya vizuri sana katika masoko mengine kama vile India, Pakistan, Thailand, Colombia, na Ukraine. Kampuni imetengeneza uwepo mkubwa wa kidunia kwa zaidi ya wasambazaji 2,000 na vituo vya huduma vya mauzo.
Kwa asili ikiwa imetengenezwa kwa ajili ya masoko ya Afrika, kwasasa TECNO inakuwa bidhaa ya kimataifa kati ya kundi la bidhaa za simu za mkononi.
TEKNOLOJIA
Barani Afrika ambako TECNO ndo iliuza simu zake za kwanza, kampuni inatambua kuanzia mwanzoni kabisa kuwa ili mtu aweze kupata mawasiliano kokote aendako alihitaji kuwa na laini tofautitofauti kulingana ili kuepuka shida ya kimtandao.
Na kuwa na simu zaidi ya moja kuweka laini tofautitofauti ni gharama kwa watumiaji.
Hivyo, TECNO ilitambua hali hii na hivyo kwa mara ya kwanza ilizindua simu ya laini mbili mnamo mwaka 2007, ni kama miaka miwili kabla ya wapinzani wake kwenyesoko.
TECNO inatambua kuwa uwepo wake mkubwa katika soko la Afrika kunaipatia kampuni hiyo uelewani nini watumiaji wanahitaji kwenye simu za kiganjani.
TECNO pia inatambua mahitaji tofauti yasoko; kwa mfano lugha za nchi tofautitofauti ziko kwenyesimu za TECNO, na hata katika kutambua nakukidhi soko la nchi ya Ethiopia kwa kuweka lugha asili ya Amharic.
Na bei za simu za TECNO ni chini ya bei za simu nyingine kwa asilimia 10.
Sifa mojawapo pekee ya simu za TECNO ni kwamba zimepewa uwezo wa kamera.
Kwa kutambua watumiaji wa simu wa Afrika simu janja hizo za TECNO zinapiga picha zenye muonekano mzuri, na hasa kipindi cha usiku na katika mazingira yenye mwangahafifu.
TECNO ilitengeneza simu zenye uwezo mkubwa wa camera ziitwazo CAMON ambazo zina kamera ya mbele nanyuma inayopiga picha nzuri kwa muonekano mzuri wangozi na pia inatumia Artificial Intelligence (AI) kutambua eneo la picha.
Suala la tatizo la umeme kwa nchi za Afrika likowazi, na hivyo TECNO inatumia teknolojia ya kuwezesha betri la simu kufanyakazi kwa muda mrefu bila kuchaji. Imetengenezwa kwa vifaa ambavyo hutumia umeme mdogo.
Ikiwa nchi duniani zinaenda kukuza mauzo ya simu za kiganjani kutokana na kupungua kwa ugonjwa wa Corona nakuondoa sheria yakutotokanje, Glocalization ni muhimu kwa bidhaa kuuzika.
Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywana Mason Group, ambayo ni kampuni ya ushauri ulimwenguni inayojikita kwenye maswala ya teknolojia ya simu, inatazamiwa kuwa mauzo yasimu za kiganjani duniani yatakuwa makubwa kwenye masoko ya Asia Pacific na Kusini mwa Jangwa la Sahara kufikia mwaka 2024.
“TECNO inajidhatiti kuleta simu janja bora na zenye teknolojia ya kisasa kwa watumiaji katika soko lenye bei shindani. Kutokana na kujidhatiti huku tumekuwa tukiwekeza kwa kiasi kikubwa ili kuongeza ubunifu kwaajili ya watejawetu”, Eric Mkomoye, Meneja Uhusianowa TECNO, amesema.