×

Shigongo Aahidi Kuliondoa Daraja la Miti Luhorongoma – Video

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, amesitisha kampeni zake kwa muda baada ya wananchi wa Kijiji cha Luhorongoma, Kata ya Kafunzo, kumtaka atembelee daraja la miti ambalo wanalitumia kuvuka kwenda ng’ambo na kutozwa fedha.

 

Shigongo amefika eneo hilo na kujionea hali halisi ya daraja hilo na mateso wanayopata wananchi wa eneo hilo ikiwemo kutozwa Tsh 1,000 mpaka Tsh 200, ambapo amehakikishia kuwa endapo atachaguliwa, daraja hilo litakuwa kilio chake bungeni kwa kushirikiana na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Msukuma, (endapo naye atashinda) ili wajenge daraja hilo na kuondoa kabisa adha kwa wananchi wa eneo hilo.

 

“Hii kazi inawezekana, tutapambana daraja hili lijengwe, Mheshimiwa Rais ni msikivu, mnyenyekevu, na anayajua matatizo ya Watanzania, yawezekana akawa hajui kama watu wa Kafunzo mnapata adha hii, nina uhakika tutamfikishia na tutapambana na TARURA ili daraja hili lijengwe na shida hii ibaki kuwa historia,” alisema Shigongo.

 

Leave a Comment