×

Radi Yaua Mahabusu, Yajeruhi Wafungwa Wanne – Video

Mahabusu mmoja wa kesi ya mauaji, Mussa Haji (25), kabila Mkurya, amefariki dunia baada ya kupigwa na radi katika Gereza wilaya ya Kibiti (Gereza la Mng’alu) huku wafungwa wengine wanne wakijeruhiwa jana Oktoba 3, 2020 kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, ACP – Onesmo Manase Lyanga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa sita mchana katika gereza hilo wakati wafungwa na mahabusu wakiwa katika ukumbi wa kupumzikia.

 

Aidha, Kamanda Lyanga amesema wafungwa waliojeruhiwa katika tukio hilo waliwahishwa hospitali na kwamba hakuna mfungwa aliyetoroka.

 

Leave a Comment