×

Benki ya Akiba Ilivyoshiriki Tamasha La Wamama Wajasiriamali wa Goba

Kina mama wa Goba wakiwa kwenye jambo lao.

Benki ya Akiba Commercial jana ilishiriki kwenye tamasha la Wamama Wajasiriamali waishio Goba Jijini Dar.

Katika tamasha hilo lililofanyika ukumbi wa Braggin uliopo Goba Center baadhi ya wamama hao walionesha bidhaa zao wanazouza.

Mhudumu wa ACB akimhudumia mmoja wa wamama waliohudhuria tamasha hilo.

Wakati kinamama wakionesha bidhaa hizo maofisa wa benki ya Akiba nao walikuwepo kuwaelimisha kinamama hao jinsi ya kutunza pesa zao kiuhakika.

Maofisa wa ACB walitumia nafasi hiyo kuwaelimisha mambo mbalimbali na kuwashauri kujiunga na benki hiyo ambayo ina akaunti mbalimbali kama vile akiba ya malengo iitwayo (LIP) ambayo inamuwezesha mwenye akaunti kujiwekea akiba kwaajili ya malengo maalum.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo, Dkt. Avemaria Semakafu akizungumza na wamama hao (hawapo pichani).

Akizungumza katika tamasha hilo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa ACB, Innocent Ishengoma aliutangazia umati wa kinamama hao huduma yao mpya ya kulipia malipo ya serikali kama vile bili za umeme, maji, faini za trafiki, kodi za majengo na malipo mengine.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki Akiba Commercial (ACB) Innocent Ishengoma akizungumza kwenye tamasha hilo.

Ishengoma aliwashauri kina mama hao kufungua akaunti kwenye benki hiyo kwa ajili ya kujipatia huduma hizo kwa ajili ya maendeleo.                                                                                                                            HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment