Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 18, 2020 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba maalumu ya Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Ujenzi wa Nyumba hiyo inajengwa na serekali kwa mujibu wa Sheria namba 3 ya Mwaka 1999 inayo ainisha ujenzi wa Nyumba maalumu kwa ajili ya makazi ya waheshimiwa Marais Mara wanapo Staafu.



