JESHI la Polisi wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kukamatwa kwa watu watatu kwa tuhuma za kuchoma moto bweni la kulia chakula la wanafunzi wa madrasa lililopo ndani ya msikiti wilayani humo.
Bweni hilo liliungua kwa moto siku mbili zilizopita ikiwa ni tukio la pili baada ya mabweni ya wanafunzi wa kike katika shule ya Kaloleni Islamic iliyopo Wilayani Moshi kuungua siku tatu zilizopita.
Mkuu wa Wilaya wa Hai, Lengai ole Sabaya, na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo walifika eneo la tukio na kuvitaka vyombo vya dola kuweka nukta katika matukio hayo yanayoonekana ya kuratibiwa na kupangwa na kwamba katika wilaya hiyo litakuwa tukio la kwanza na la mwisho.
View this post on Instagram
