HUENDA kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos, akaukosa mchezo wa leo Alhamisi, Oktoba 22, 2020, dhidi ya Polisi Tanzania kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha ya enka.
Rekodi zinaonyesha kuwa yeye ni kinara wa pasi za mwisho ndani ya Yanga iliyofunga mabao 7 akiwa nazo mbili na amefunga bao moja.
Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni na utakuwa wa Kwanza kwa Cedric Kaze baada ya kubeba mikoba ha Zlatko Krmpotic.
Polisi Tanzania watamkosa moja kwa moja mshambuliaji wao Daruesh Saliboko ambaye alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Gwambina FC. Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Amri Abeid ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
