×

Video: Rais Magufuli Azindua Safari Za Treni Dar-Tanga-Arusha

RAIS Magufuli leo Oktoba 24, 2020 amezinduzi rasmi wa treni ya abiria inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Arusha kupitia Moshi na Tanga iliyokuwa imeacha kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 30.

“Leo nimefurahi sana kuja hapa stesheni ya Arusha kuzindua usafiri wa reli kutoka DSM, Tanga, Korogwe hadi Arusha ambao ulikuwa umesimama kwa miaka 30. Miundombinu ya usafiri ni kichocheo kikubwa cha ustawi wa shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii, biashara nk”

“Ukosefu au ubovu wa miundombinu ya usafiri ni kikwazo kikubwa cha ustawi wa shughuli za kiuchumi. Tafiti zinaonyesha ukosefu ama ubovu wa miundombinu ya usafiri unapunguza pato la nchi za Afrika kwa 2% na kuongeza bei ya bidhaa kwa 40%” -JPM akiwa Arusha

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiongoza Brass Band ya polisi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Safari za treni kutoka Dar es salaam, Tanga na Arusha unaofanyika leo Jumamosi Oktoba 24, 2020 hi jijini Arusha ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. John Pombe Magufuli kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.

Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla hiyo inayofanyika jijini Arusha ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli atazindua safari za treni Kati ya Dar es salaam, Tanga na Arusha.
Wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro Anna Mghwira, Martine Shigella Tanga na Joseph Mkirikiti Manyara wakiwatunza wanamuziki wa Brass Band ya Polisi wakati wakitumuiza katika hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Ndugu Kenani Kihongosi akiimba wimba maalum aliomtungia Rais Dk. John Pombe Magufuli katika uzinduzi wa Safari ya treni ya TRC Kati ya Dar es salaam , Tanga na Arusha leo jijini Arusha.
Viongozi mbalimbali wa dini wamehudhuria katika hafla hiyo.

Leave a Comment