RAIS Dkt John Magufuli, leo Oktoba 26, amezindua msikiti uliopo Chamwino mkoani Dodoma, ambapo tukio hilo limeshuhudiwa na Mufti mkuu wa Tanzania, Aboubakary Bin Zubeir, pamoja na viongozi wengine wa dini.
“Watanzania hatuna ubaguzi wa dini, kabila wala rangi, Agosti 23 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Kanisa Kataliki Chamwino, niliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti huu hii ni baada ya kuona ni mdogo na ulikuwa umeanza kuchakaa.
“Niwashukuru wote waliojitokeza kuchangia ujenzi wa Msikiti huu, kwa yeyote aliyechangia Msikiti huu asijione amepoteza, amefanya jambo zuri sana ambalo lina ujira mkubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu,” amesema Magufuli.
Aidha, Rais ameahidi kuwa baada ya kukamilika kwa msikiti huo, sasa atasaidia ujenzi wa makanisa mengine ili Chamwino ambapo ni makao makuu yawe na makanisa makubwa kwa ajili ya waumini wa dini husika kuabudia.


