KAMANDA wa Polisi Kanda Maaalum ya dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amewaonya wanasiasa walioshindwa chaguzi kwenye mikoa mingine na sasa wanataka kufanya maandamano Dar es Salaam kuwa mkoa huo si shamba la bibi. Amesema muda wa kampeni umekwisha, waheshimu matokeo na atakayeandamana asilaumu kitakachompata.
