
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Infinix mbioni kutamba tena na toleo la NOTE na hii ni baada ya toleo la awali la Infinix NOTE 7 kufanya vizuri sokoni. Kupitia mtandao wao @infinixmobiletz wameashiria kuna ujio wa simu mpya yenye sifa zifuatazo;
- Helio G80 processor
- 64MP Ultra HD 6 kamera
- 5200mAh battery.
Huku ikiwa kampuni haijataja ni toleo gani hilo lakini wadau wa simu za Infinix wamekuwa wakitabiri huwenda toleo hilo jipya ni Infinix NOTE 8 na kutokana na baadhi ya sifa zilizotajwa hapo juu. Inasemekana toleo la NOTE ni moja ya toleo lenye ubora kama ilivyo kwa toleo la Infinix ZERO.
Tukiwa bado hatujafahamu sifa nyingine za simu hiyo inayosemekana huenda ni Infinix NOTE 8 lakini tunafahamu Infinix ni kampuni imara yenye kuzalisha simu zenye viwango vya hali ya juu kwa bei ambayo Mtanzania mwenye uchumi wa hali yoyote anaweza kuimudu.

Kwa uchache wa sifa tulizozinyaka inaonekana simu hiyo itakuwatishio kutokana na aina ya processor Helio G80 kuwa processor yenye kuhimili application zenye ujazo wowote. Processor ya Helio G80 pamoja ya kuhimili application zenye ujazo mkubwa lakini pia inapunguza kasi ya simu kuisha chaji, inazuia simu isipate moto kwa matumizi ya muda mrefu na kuziendesha application kama za games na nyinginezo pasipo kuzembeazembea.
Bado maswali yanabaki kwetu hadi pale tutakapompata Aisha Karupa Afisa wa Uhusiano wa Kampuni ya Infinix azungumze nasi simu hiyo ni simu gani na sifa nyingine za simu hiyo na bei yake.