
KUNDI la Vuvuzela Classic Modern Taarab usiku wa kuamkia jana iliwanyongesha mauno kinamama waliohudhuria onesho lililofanyika Ukumbi wa Open Air uliopo Kawe Jijini Dar.

Kundi hilo linaloongozwa na Aisha Othman a.k.a Vuvuzela lilipiga shoo kali ukumbini hapo na kuwafanya wamama waliofurika ukumbini hapo kukata nyonga za hatari bila huruma.
Mpiga kinanda Omary Kisila akifanya yake katika kunogesha mambo.
Mpiga kinanda mahiri wa kundi hilo Omary Kisila na wenzake walifanya kazi pevu ya kuwadatisha wamama hao na kuwafanya wakate nyonga bila kuchoka.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

