Timu ya Yanga leo Novemba 3 imelazimishwa sare bila kufungana dhidi ya Gwambina katika mfululizo wa mechi za ligi kuu Tanzania bara, mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Gwambina Complex, jijini Mwanza
kwa mara ya kwanza Yanga wanadondosha pointi Kanda ya Ziwa msimu huu
Kocha Cedric Kaze aliamua kuwapumnzisha nyota wake wengi kwa ajili ya mechi ijayo ambayo wanakutana na watani zao Simba hali ambayo kwa kiasi kikubwa imechangia matokeo ya leo.
Sare hiyo imeipeleka kileleni mwa msimamo wa ligi wakioongoza kwa pointi 23 na baada ya michezo tisa wakiwaacha Azam Fc kwa pointi moja.
Kwenye mchezo huo ulilazimika kusimama baada ya nyuki kuingia uwanjani na kulamisha mchezo kusimama kwa dakika kadhaa.
Bado ukuta wa Yanga unaonekana kuwa mgumu kwani mpaka sasa umeruhusu magoli mawili tu huku akiwa na ‘clean sheet’ saba.

