POLISI mkoani Shinyanga imewakamata watu tisa kwa tuhuma za kutaka kuchoma moto nyumba ya mbunge mteule wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Miongoni mwa watuhumiwa ni aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salome Makamba, ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana.
Watuhumiwa wengine ni wanaume wanane wanaoendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika, watawafikisha mahakamani.
