×

Petrol Yapanda Bei, Dizeli Yashuka

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa bei mpya za mafuta ya dizeli na petroli zitakazoanza kutumika kuanzia Novemba 4, 2020.

Dar es Salaam bei za rejareja ya petroli imeongezeka kwa Tsh 25 kwa kila lita na bei ya mafuta ya aa imeongezeka kwa Tsh 12 kwa lita huku bei ya dizeli ikiwa imeshuka kwa Tsh 44 kwa lita.

Bei ya jumla kwa Dar kwa petroli imepanda kwa Tsh 28.07 kwa lita, bei ya mafuta ya taa imeongezeka kwa Tsh 14.95 kwa lita huku bei ya dizeli ikiwa imepungua kwa Tsh 41.32 kwa lita.

EWURA imesema mabadiliko haya ya bei yanatokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia la mafuta.

Leave a Comment