×

Watoto wa Trump Waitupia Lawama Republican

WATOTO wawili wa kiume wa Rais wa Marekani Donald Trump wamekishutumu chama cha Republican kwa kutokuwa bega kwa bega na baba yao, kipindi hiki  ambacho yupo kwenye wakati mgumu kutetea kiti chake.

 

Trump Don Jr ambaye ni mkubwa amekosoa chama hicho na kukiita dhaifu, wakati mdogo wake Erick Trump akisema kitendo cha chama kutomuunga mkono Trump ni kuwavunja moyo wanachama wake na kuwafanya kuwanyonge.

 

Hatua hiyo ni ishara tosha kuwa  na mgawanyiko ulioibuka baina ya washirika wa Trump ndani ya chama huku wengine wakishutumiwa kwa usaliti.

 

Ushindani mkali umeshuhudiwa lakini mgombea wa Democratic Joe Biden ambaye anapewa nafsi kubwa ya kushinda uchaguzi huo.

Leave a Comment