BEKI wa kati wa klabu ya Liverpool, Joe Gomez, ameripotiwa kupata majeraha makubwa na anatazamiwa kukaa nje kwa muda mrefu.
Gomez ameumia akiwa katika timu ya taifa ya England, inayojiwinda na michezo kadhaa wiki hii, ukiwemo ule wa kirafiki dhidi ya North Ireland utakaopigwa leo (Alhamisi) Novemba 12, 2020, ambapo kocha mkuu wa England, Gareth Southgate, amesema ”majeraha yake ni makubwa lakini bado sifahamu itamchukua muda gani kukaa nje ya uwanja. Jambo hili limenihuzunisha sana, kwa kuwa alikuwa sehemu ya mipango yangu.”
Kwa Liverpool na kocha wao, Jurgen Klopp, taarifa hiyo si nzuri hata kidogo, kwa kuwa safu yake ya ulinzi imekumbwa na majeruhi wengi yanaowalazimu baadhi ya nyota wake kutoonekana kwa muda mrefu uwanjani, akiwemo Virgil van Dijk na kiungo Mbrazil ambaye amekuwa akichezeshwa katika safu ya ulinzi kama mbadala wa Van Dijk.
Kukosekana kwa wachezaji hao watatu muhimu katika kikosi cha Liverpool — Van Dijk, Fabinho na Joe Gomez — kunauweka ubingwa rehani ubingwa walioutwaa msimu wa 2019-2020.
