×

Watanzania Watakiwa Kupima Afya Zao Kila Mara Kudhibiti Kisukari

Mkurugenzi wa Abel & Fernandes, Fatma Fernandes akimchukua maelezo mmoja wa waliojitokeza kupima afya zao.

Chukua hatua leo, badilika kesho… Kisukari; Wauguzi kwa mageuzi katika sekta ya afya.

Maadhimisho ya Siku ya Kisukari hapa nchini ni mojawapo ya miradi ya uwajibikaji kwa jamii inayotekelezwa na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications pamoja na Quincewood Consulting.

Daktari akimpima jamaa aliyekwenda kucheki afya yake.

Katika maadhimisho ya mwaka huu hapa Tanzania, kampuni hizi zimeungana na Hospitali ya Kisukari na Moyo St. Laurent kuandaa maadhimisho haya ya kisukari duniani ambayo yanafanyika Novemba 14 mwaka huu.Kampuni ya Abel & Fernandes Communications pamoja na wadau wengine tunaungana na Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Kisukari kwa kujenga uelewa kuhusu ugonjwa huo ambao kwa mujibuwa takwimu za wizara ya afya hadi sasa umeathiri zaidi ya watu milioni 1.5 nchini.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Kisukari ya St. Laurent Dkt. Maria Maige akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Kauli mbiu yamaadhimisho ya Kisukari duniani  kwa mwaka huu ni “Wauguzi kwa mageuzi katika sekta ya afya na Kisukari”. Kampeni hii inalenga kuwapa motisha wauguzi kutekeleza majukumu yao kwa uweledi ili kuwapatia huduma bora, stahiki na zenye staha wagonjwa wa Kisukari nchini.

Wauguzi wanahesabika kuwa nusu ya wafanyakazi wote wa sekta ya afya nchini. Ni kada mojawapo inayoweza kuwapatia huduma bora watu wanaoishi na magonjwa mbalimbali. Watu wanaoishi na Kisukari huhitaji zaidi msaada wa wauguzi katika kutibu tatizo hilo.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Maradhi ya Kisukari (IDF)  “Waathiriwa wa Kisukari hukumbana na changamoto mbalimbali hivyo elimu ndio kiungo muhimu katika kuwaunga mkono wauguzi. Wakati namba za waathiriwa wa Kisukari zikizidi kuongezeka, majukumu ya wauguzi na watumishi wengine wa sekta ya afya ni muhimu katika kukabiliana na hali hiyo.

Zoezi la upimaji ukiendelea.

Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kwa pamoja tunaungana na wauguzi kuzuia na kutoa muongozo kuhusu Kisukari, pia tunatoa huduma kwa mamia ya jamii kwa malengo ya kuwapatia taarifa muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna ya kukabiliana nao.

Serikali ya Tanzania imetambua umuhimu wa kuwekeza katika elimu na mafunzo ambayo yatatoa wataalam sahihi lakini pia kuongeza wauguzi bora watakaotoa huduma bora kwa watu walioathiriwa na Kisukari.

Wakati zoezi likiendelea Mkurugenzi wa Abel & Fernandes, Fatma Fernandes naye aliangaliwa afya yake kwanza.
Kupima uzito nako ni jambo muhimu sana.

“Hii ni siku muhimu kwetu wote ambayo inatoa fursa ya kupata huduma za afya bure kwa malengo ya kuboresha afya za watanzania wanaoishi na Kisukari, pia kuboresha maisha ya watu wanaoishi na ugonjwa huo. Huduma hizi zitaanza kutolewa kuanzia saa mbili asubuhi, kwa mazoezi mepesi yatakayo sindikizwa na vipimo vya bure pamoja na michezo ya watoto yenye kuvutia,” alisema Fatma Fernandes, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Abel & Fernandes.

Mkurugenzi wa Abel & Fernandes, Fatma Fernandes (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Kisukari ya St. Laurent, Dkt. Maria Maige (kushoto) wakibadilishana mawazo na wawakilishi wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Johari Yusufu mwenye miwani na Kulwa Kaombwe.
Wadau wakionesha fulana yenye ujumbe wa masuala ya afya.

Katika kutekeleza malengo ya kauli mbiu ya siku hii ya kisukari duniani, “Wauguzi kwa mageuzi katika Sekta ya afya,” kutakuwepo na wauguzi kutoka Hospitali ya Laurent, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) sambamba na huduma za ushauri wa bure wa kitabibu.

Wadau katika picha ya pamoja.

Ungana nasi Jumamosi hii, Novemba 14, 2020 katika Hospitali ya Kisukari na Moyo Laurent. Hospitali hii ipo karibu na mzunguko wa njia panda Kawe. Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa baruapepe; [email protected]

Leave a Comment