×

Metacha Mnata Amempoteza Manula

METACHA Mnata, kipa namba moja ndani ya Yanga, amempoteza jumla kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kwenye idadi ya mabao ya kufungwa, kukusanya clean sheet pamoja na dakika za kucheza msimu wa 2020/21.

 

 

Simba na Yanga zikiwa zimecheza mechi 10 za Ligi Kuu Bara, Metacha ameanza kwenye mechi tisa akikosekana kwenye mchezo dhidi ya Prisons uliokamilika kwa sare ya bao 1-1.

 

 

Nafasi yake ilichukuliwa na Faroukh Shikhalo. Kipa huyo alikaa langoni kwenye michezo hii; Yanga 1-0 Mbeya City, Kagera Sugar 0-1 Yanga, Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Yanga 3-0 Coastal Union, Yanga 1-0 Polisi Tanzania, KMC 1-2 Yanga, Biashara United 0-1 Yanga, Gwambina 0-0 Yanga na Yanga 1-1 Simba.

 

 

Kwenye mechi 10 ambazo ni sawa na dakika 900, Metacha amekosekana kwa dakika 90, hivyo ametumia dakika 810 kukaa langoni na ameruhusu mabao mawili akiondoka na clean sheet saba. Kwa upande wa Manula, Simba ikiwa imecheza mechi 10, ameanza langoni kwenye mechi saba, tatu alikaa Beno Kakolanya.

 

 

Mechi alizozikosa Manula, matokeo yalikuwa hivi; Simba 0-1 Ruvu Shooting, Simba 5-0 Mwadui na Simba 2-0 Kagera Sugar. Manula alicheza mechi hizi; Ihefu 1-2 Simba, Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Simba 4-0 Biashara United, Simba 3-0 Gwambina, JKT Tanzania 0-4 Simba, Tanzania Prisons 1-0 Simba na Yanga 1-1 Simba.

 

Akiwa amekaa langoni mechi saba, Manula amefungwa mabao manne na katika dakika 900 sawa na mechi kumi, ametumia dakika 630 akiondoka na clean sheet tatu.

~LUNYAMADZO MLYUKA, DAR

Leave a Comment