
KAMPUNI ya Global Group inamiliki, miongoni mwa makampuni mengine, chombo cha habari chenye nguvu na umaarufu, ndani na nje ya Tanzania, kinachoitwa GLOBAL PUBLISHERS & GENERAL ENTERPRISES LIMITED.
Kampuni hii imejikita katika majukwaa makuu manne ya upashaji habari ambayo ni Magazeti, Televisheni na Radio ya Mtandaoni pamoja na Mitandao ya Kijamii.
Global imekuwa katika tasnia ya habari na utangazaji wa biashara za makampuni mbalimbali kwa zaidi ya miaka 20 sasa.