×

Shangwe Shangwena Yaanza Kugawa Gari na Pesa Kwa Wateja

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom PLC, Jacquiline Materu akizungumza kabla ya kuanza kuchezesha bahati nasibu hiyo kushoto ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Rasul Masoud.

Mkazi wa Biharamuro mkoani Kagera Happyness Manembe anayejishughulisha na kilimo, leo ameibuka mshindi wa gari aina ya Renault mpya katika promosheni ya Shangwe Shangwena inayoendeshwa na kampuni ya mawasilino ya Vodacom PLC.

 

Sambamba na mkulima huyo kuibuka na gari hiyo wateja wengine watano wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja.

Wanahabari wakihakikisha wanachukua matukuo ili kuwaonesha wananchi mambo yalivyokwenda kiukweli na uwazi.

VODACOM PLC imeanza kuwapa zawadi za Sikuu ya Krisimasi wateja wake wanaotumia huduma mbalimbali za kampuni hiyo haswa M-Pesa, kama vile kuweka pesa, kutuma pesa, kulipia bili na nyinginezo.

Mchakato wa kuwapata washindi hao ulifanywa na maofisa wa Vodacom PLC kwa kutumia program ya kompyuta kwa usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.

 

Katika mchakato huo, ndipo mkulima huyo akaibuka na gari hiyo huku wateja wengine, David Daniel (45) mkazi wa Njombe, Zainab Bakari (21) mkazi wa Kwimba Mwanza, Ashura Elisha (45) mkazi wa Kibaha Pwani, Gabriel Reginald wa Tegeta Dar na Jalife Juma (70) mkazi wa Tanga wao walijipatia shilingi milioni moja kila mmoja.

 

Akizungumza na wanahabari baada ya kuwapata washindi hao, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom PLC, Jacquiline Materu amewataka watumiaji wengine wa simu kutumia huduma za kampuni hiyo ili nao kuweza kuibuka na zawadi hizo na kuweza kuambulia magari manne yaliyobaki ambayo yanatarajiwa kutolewa kabla ya Krisimasi.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Vodacom PLC, Nandi Mwiyombella (katikati) Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu na Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Rasul Masoud wakifurahia baada ya kumpata mshindi wa gari.

“Tunawaomba wateja wetu waendelee kutumia huduma zetu za M-Pesa ili kuweza kujishindia zawadi hizo ambapo ukitumia tu huduma hizo unakuwa tayari umeingia kwenye kinyang’anyiro hicho na muda wowote unaweza kupigiwa simu na kujulishwa ushindi wako kama ilivyokuwa kwa Happyness”. Alimaliza kusema Jackline.

 

Washindi wa zawadi ya milioni moja baada ya kupatikana walipigiwa simu na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu na alipopatikana mshindi wa gari alipigiwa simu na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella aliyewawakilisha viongozi wa kampuni hiyo.

Leave a Comment