×

Reekado, Harmonize Mguu kwa Mguu

STAA wa muziki kutoka Nigeria, Reekado Banks ameachia singo mpya inayokwenda kwa jina la Mama akiwa amemshirikisha Mbongo Fleva, Harmonize.

Kazi hiyo mpya iliyopandishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza juzi Novemba 27, mwaka huu imetayarishwa na prodyuza mkali, Tee Y Mix na ndani yake Reekado na Harmonize wanaonekana kwenye mandhari tofauti, kabla ya wenyewe kusema “Tanzania na Nigeria ni nyumbani”.

 

Akizungumzia singo hiyo, Reekado anasema: “Kaka yangu Harmonize amefanya makubwa kwenye kibao changu ‘Mama’ ni wimbo mkali zaidi wenye mahadhi ya Kiafrika, ambao mtu yeyote mahali popote barani Afrika na kwingineko ataunganishwa na kujisikia yupo Afrika.

Mama Official Audio on YouTube

“Nilifikiria sana kuhusu ni nani ambaye angefaa kushiriki katika wimbo huu, nikamuona Harmonize. Nilipozungumza naye, mara moja alikuja Lagos (Nigeria), tukaingia studio na kufanya kazi. Ni kazi bomba.”

 

Aidha, Reekado pia amepata kushirikiana na msanii mwingine wa Afrika Mashariki, Otile Brown kutoka Kenya.

 

Wimbo huo upo ndani ya EP mpya ‘Off The Record’ ambapo nyimbo nyingine ni pamoja na Need More aliomshirikisha Kida Kudz na EO, Happy Yourself, Rora, Speak To Me aliomshirikisha Tiwa Savage, You Dey Mad aliopiga kolabo na Atti Faya na People Dey aliomshirikisha Mr Eazi.

Akigonga msumari wa mwisho, Reekado anasema: “Unajua kufanya kazi na wasanii Harmonize, Tiwa na Eazi ni kuongeza wigo wa mashabiki, maana nina uhakika mashabiki wao watasikiliza na watakuwa mashabiki wangu pia. Kadhalika mashabiki wangu watakuwa wao.

“Umekuwa mwaka mzuri kwangu, kwa kazi nzuri ya kuvutia inayoelezea maisha na utamaduni wa Kiafrika, naahidi mwaka 2021 tutafanya makubwa zaidi.”

 

Leave a Comment