
Toleo jipya la simu ya Infinix 8 Note iliyozinduliwa hivi karibuni imebeba processor aina ya Helio G80 ikiwa ndio sifa kuu kwa simu hiyo na kupelekea kuvunja rekodi yake yenyewe kwa kuja na simu janja yenye mfumo wa kukidhi mahitaji ya wadau wenye matumizi makubwa ya simu.
Akizungumza na wanahabari Afisa Uhusiano wa Infinix Tanzania, Aisha Karupa amesema Infinix NOTE 8 imekuja na sifa nyingine zenye kuifanya simu hiyo kuwa ya kipekee kama vile 64MP Ultra HD 6, BatterymAh 5200, kioo cha nchi 6.95, Android 10.
Processor
MediaTek Helio G80 processor ikichagizwa na MediaTek HyperEngine Game Technology ambayo inaipa nguvu simu hiyo na kuiwezesha kufanyakazi kwa haraka na kuhakikisha kuwa simu hiyo inagusa maeneo mengine yote ya kimsingi kwa ufanisi. Chipset yenye sifa ya kufanyakazi vizuri imefungwa katika simu hiyo si tu kuifanya iwe nyepesi wakati wa matumizi bali inaifanya kuwa imara zaidi. Amesema Aisha.
“Inarahisisha games zinazochukua muda mrefu kufunguka kwa haraka na kucheza kwa ufanisi, zinatumika katika maeneo maalum na games zenye ukubwa. Simu hii imeongezewa ufanisi wa hali ya juu na maboresho ya uunganishwaji kwa minajili ya kuwezesha mtu kucheza game bila bughudha”.
Battery

Infinix NOTE 8 imebeba ujazo wa battery yenye mAh 5200 Mlengo ni kuona mtumiaji wa Infinix Note 8 anaifurahia simu yake kwa muda mrefu pasipo hofu ya kuzima chaji lakini pia hujaa chaji kwa haraka. Hii inapewa nguvu nateknolojia ya hali ya juu (power marathon) iliyomo ndani ya simu janja ambayo hata kama chaji inakwisha inaiwezesha kutunza chaji kwa muda fulani. Kwa wapenzi wa games, hii itawahakikishia wanakuwa na muda mrefu wa kucheza au kutazama na kwa mfanyabiashara au mjasiriamali aliyefanikiwa, Note 8 inakupa uhakika wa haya yafuatayo kwa urahisi kama vile kutuma barua pepe, kutumia apps zinazohusu shughuli za kiofisi, kutumia apps za kufanya mikutano kupitia video na mengine zaidi.

Vile vile simu hii inateknolojia ya injini mbili. Jambo hili linaifanya Infinix Note 8 kuwa ya baridi, ikipunguza joto kwa jotoridi 8 wakati inachajiwa.
Kamera
Moja ya sifa kubwa zinazoitofautisha simu hii na simu nyingine ni kuwa na kamera kubwa mbili 64MP Ultra HD 6nyuma na 16MP mbele. Kioo chake kikiwa na uwiano wa 20.5:9ambacho kina kamera ndogo mbili ambapo inakiwezesha kioo cha simu hiyo kuzunguka kufikia eneo la kamera kiasi cha kutoleta usumbufu ukiitumia kuangalia video kwenye simu.
Simu hiyo yenye kioo chake cha kisasa (6.95″ Dual Infinity-O Display) kinasaidia kamera kuchukua picha zenye ubora kwa kuhakikisha hakuna vizuizi vyovyote vitakavyo haribu ubora wa picha.
Infinix pia imepata suluhisho la kukabiliana na mazingira ya mwanga mdogo mbalo limekuwa likiwasumbua watumiaji wakati wa kuchukua video. Kwa kutumia zaidi ya siku 180 (usiku na mchana) kufanya utafiti na maboresho kukabiliana na suala hili, simu hii ina mfumo maalumu wa kuiwezesha simu kufanyakazi katika mazingira ya giza (Note 8’s Ultra Night Mode 2.0) inakupa matokeo mazuri katika mazingira yenye mwanga hafifu.
Muonekano

Muonekano wake utaweza kuwavutia watu mbalimbali na kwa namna simu hii ilivyo umuhimu wake utaongezeka maradufu kama ambavyo ilivyo muhimu kwa mtu kuvaa nguo mwilini mwake. Simu hii inamuundo mwepesi sambamba na GEM CUT ambayo imebuniwa kwa kuangalia mitindo inavyokwenda na hadhi yake. Uumbaji wa simu hii ambao bado ni mfano wa kuigwa umebebwa na mistari ya kipekee na uhalisia wa teknolojia. Muundo wake wa Gem Cut ni mahususi kwaajili ya kubadili muonekano wa mtumiaji.
Mapokezi
Ukipitapita madukani na kwenye mitandao ya kijamii utagundua ni simu iliyopokelewa vizuri sana na hii huenda wanachokipromoti ndicho wateja wanachokutana nacho baada ya ununuzi, Infinix NOTE 8 imepokelewa vizuri na watu wa rika lote hasa wale wenye kuitumia simu kama chombo muhimu katika shughuli za kila siku za kujipatia kipato.
Upatikanaji
Infinix NOTE 8 inapatikana kwa bei isiyozidi sh. 540,000 katika maduka yote ya simu nchini Tanzania ikiwa na ofa ya GB 96 kutoka Vodacom lakini pia unaweza tembelea https://www.infinixmobility.com/tz/ . Alimaliza kusema Aisha.