The House of Favourite Newspapers

Marekani Yaripoti Vifo vya Corona 2,700 kwa Siku Moja

0

RIPOTI kutoka Marekani zinasema watu 2,700 wameripotiwa kufa kwa siku moja ya Jumatano (Desemba 3, 2020) pekee ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi cha vifo kuwahi kuripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huo nchini humo.

Watu 100,000 wamefikishwa hospitali kwa ugonjwa huo katika kipindi cha siku moja huku wengine 200,000 wakiripotiwa kuwa na maambukizi mapya nchini humo.

Wakazi wa jiji la Los Angeles wametakiwa kukaa ndani kutokana na ongezeko la ugonjwa huo huku wakitakiwa kuchukua hatua zaidi za tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

Nchini Brazil katika kipindi cha saa 24 zilizopita zaidi ya watu 50,000 wameripotiwa kufikishwa hospitali wakiwa na ugonjwa wa Covid 19.

Waziri wa Afya nchini Marekani, Alex Azar,  amesema chanjo ya Covid 19 inatarajiwa kuanza kutumika nchini humo wiki ijayo.

Leave A Reply