×

Riyama Aanika Kinachomkosha kwa Mumewe

MUIGIZAJI Riyama Ally kwa mara ya kwanza ametaja siri ya kitu asichokipenda mume wake, Haji Mwalimu Mzee ‘Leo Mysterio’ kuwa ni kumuona akiwa na majonzi.

 

Akizungumza na Risasi, mwanamama huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwa kuvaa uhalisia vilivyo katika filamu mbalimbali alizocheza, alisema kuwa mumewe akirudi nyumbani na kumkuta hayupo sawa basi atafanya kila awezalo ili kumfurahisha.

 

“Mume wangu ni mtu ambaye hapendi kuniona nikiwa na majonzi au mawazo ya kupitiliza, yaani atafanya vitu ninavyovipenda na kunipa furaha ili kuhakikisha nakuwa sawa,” alisema Riyama.

 

STORI: MEMORISE RICHARD

Leave a Comment