×

Mkurugenzi Geita Asimamishwa kwa Agizo la JPM – Video

WAZIRI wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,  amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Modest Joseph, ili kupisha uchunguzi na amemuagiza Katibu Mkuu, Mhandisi Joseph Nyamhanga, kutuma timu ya uchunguzi katika Mji wa Geita kuchunguza matumizi ya fedha za halmashauri hiyo.

 

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kuelezea kukasirishwa na hatua ya mkurugenzi huyo kununua gari la kifahari kwa fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya huduma za kimaendeleo kwenye halmashauri hiyo.

 

Magufuli amemtaka Jafo kuanza kazi yake ya uwaziri kwa kumwajibisha mkurugenzi huyo, kauli aliyoitoa Ikulu ya Chamwino, Dodoma wakati akiwaapisha mawaziri na wabunge leo, Desemba 9, 2020.

Leave a Comment