×

Jamii Imetakiwa Kutofumbia Macho Vitendo vya Ukatili

Spika Mstaafu Anne Makinda akizungumza kwenye mkutano huo.

JAMII imetakiwa kutofumbia macho vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikijitokeza kwani vinapunguza nguvu kazi ambayo ndiyo msingi wa maendeleo.

Akizunguza jana jijini Dar es Salaama na Spika Mstaafu Anne Makinda wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya beijin na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Alisema suala lakutokomeza ukatili ni jambo linalohitaji ushirikiano na kila mtu anapopaza sauti itasaidia kutokomeza ujatili.

“Taifa lisilo na ukatili linakuwa na maendeleo kwani kunapokuwepo na ukatili mnashindwa kufanya shughuli za kimaendeleo hivyo ni vizuri kama tutapaza sauti zetu”alisema

“Ukatili wa kijinsia ni janga linaloikabili Dunia kwa mujibu wa ofisi za takwimu nchini ya mwaka 2015 na 2016 asilimia 40 ya wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wanapigwa au kufanyiwa vitendo vya kingono.

Sehemu ya waliohudhuria maadhimisho hayo.

“Jamii inatakiwa kubadili mira na desturi ili kutokomeza ukatili hasa maeneo ya Kagera, Mara, Mwanza na Kigoma ambapo suala la ukatili limeonekana kushika kasi siku hadi siku

“Kamati zifanye kazi ipasavyo ili kuhakikisha suala hilo linakwisha kabisa na si kuyafumbia macho na wadau tutumie mpango kazi maalumu ili kutekeleza na kuzijengea uwezo kamati zinazohusika na mapambano hayo.

“Wakati ni sasa wa jamii au taasisi kuhakikisha wanaacha alamu ambayo itasaidia watoto hapo baadae kujua tumetoka wapi na tunakwenda wapi alisema.

Naye Ofisa Mkuu wa Ustawi wa Jamii, Dalius Damas ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. John Jingu alisema serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha zinatokomeza suala la ukatili wa kijinsia nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia (TGNP) Lilian Liundi akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

“Kama ambavyo tumeanza kutekeleza kwa kuwa na madawati ya kijinsia na yamefika hadi katika ngazi ya vyuo vikuu lengo letu hadi kufikia mwaka 2022 kuhakikisha tunapunguza kwa asilimia kubwa suala la ukatili kama sio kumaliza kabisa”alisema

Aidha Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia TGNP, Lilian Liundi alisema Serikali yetu imejitahidi kuweka sheria na mikakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Hivi ndivyo yalivyosomeka baadhi ya mabango kwenye maadhimisho hayo.

” Tumeona Serikali namna ambavyo imejitahidi kuweka sheria na mikakati ya kutokomeza ukatili, lakini changamoto inayofifisha jitihada hizi ni bajeti kidogo inayotengwa kuviwezesha vyombo husika.

“Tunaiomba Serikali kuu na halmashauri zetu zitoe kipaumbele kwenye bajeti zake katika kuwezesha dawati la jinsia na mtoto, polisi, kamati za utekelezaji wa mpango kazi wa kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto,” alisema.

Leave a Comment