
SIKU hizi muonekano ndio humbeba mtu hasa mtoto wa kike, ndio! Ukiwa na muonekano mzuri ni rahisi hata kupata madili ya pesa kama vile matangazo, ubalozi wa makampuni mbalimbali na kadhalika.
Ndio maana kumekuwa na tetesi nyingi sana mitandaoni zikiwahusisha baadhi ya mastaa mbalimbali duniani kuwa wamefanya upasuaji kwenye miili yao, huku lengo likidaiwa kuwa ni kutaka kuwa na mvuto zaidi hasa kwa wanaume.

Leo nakuletea orodha fupi ya baadhi ya mastaa Bongo ambao wanatajwatajwa kufanya upasuaji kutengeneza miili yao ili kuongeza shepu, matiti, midomo na vitu vingine lakini hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo na wenyewe hawajawahi kukiri hivyo kubaki tu kuwa stori za mitandaoni:
NICOLE
Jina lake halisi anaitwa Nicole Joyce Berry, alianza ku-pata umaarufu baada ya kutupia picha na video zake katika mtandao wa Instagram zi-lizomuonye-sha kuwa na shepu bomba na yenye mvuto wa hatari.
Baada ya hapo akaja kupata umaarufu mkubwa tena baada ya kushiriki kwenye wimbo wa Uno ulioimbwa na Rajab Abdul ‘Harmonize’ kama video queen.Mbali na yote mrembo huyu amekuwa akidaiwa kufanya upasuaji wa kiuno na shepu, lengo ni ili awe na kiuno nyigu chenye kumvutia kila mtu hasa watoto wa kiume.

POSHY QUEEN
Anaitwa Jackline Obed, mwaka jana zilisambaa picha zake za zamani zikimuonyesha mwembamba asiye na shepu kubwa wala hipsi pana, ghafla watu wakaanza kumuona akiwa na bonge la shepu, huku hipsi ndio usiseme zimechomoza balaa, watoto wa mjini wanakumbia anatembea na pisto.Naye ni miongoni mwa mastaa wanaodaiwa kufanya upasuaji wa makalio na hipsi ili avutie wanaume.

SARAH
Sarah Michelotti ndio jina lake halisi, alianza kupata umaarufu mkubwa baada ya kuanza kutoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’.
Mwanadada huyu naye anadaiwa kufanya upasuaji wa mwili wake wote, kuanzia sura, pua, shepu na viungo vingine kwenye mwili wake.

HAMISA MOBETO
Mbali na tetesi nyingi kumuandama kuwa anatumia mkorogo ili kung’arisha ngozi yake iwe nyeupe pee, hivi karibuni mwanamitindo huyu ameingia kwenye kashfa nzito mara baada ya wananzengo kudai alitimkia nchini Uturuki kwa ajili ya kwenda kufanya upasuaji wa kuongeza shepu na lipsi.
WEMA SEPETU
Ni msanii wa filamu nchini, mara kadhaa watu wamekuwa wakidai mrembo huyu anafanya sana upasuaji kwenye mwili wake, mwanzo walisema kuwa alifanya upasuaji wa kuongeza shepu ndio maana hapo awali alikuwa na shepu yenye mvuto wa hali ya juu.Badaaye wakadai kuwa amefanya tena upasuaji wa utumbo uliopelekea mwanadada huyu kukonda kupita kiasi.