×

Pati ya Tanasha Yamzulia Jambo Kwa Zari

UNAAMBIWA ilikuwa ni shangwe shangwena kutoka kwa msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Kenya, Tanasha Donna Oketch ambaye pia ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, lakini imemzulia jambo zito.

 

Ile shughuli yake iliyokwenda kwa jina la All White Party ambayo ni ya kufunga mwaka huu wa 2020 ilikuwa ni hatari tupu. Tanasha aliangusha pati hiyo usiku wa kuamkia Jumamosi aliyopita katika hoteli ya kifahari huko nchini Kenya inayojulikana kwa jina la Afrosayari-Ground.

Kwa mujibu wa mitandao ya Kenya, pati hiyo imezua jambo baada ya mashabiki kusema kwamba, amemuiga ‘zilipendwa mwenzake’ kwa Diamond au Mondi, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa sababu miaka michache iliyopita alifanya pati kama hiyo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

 

“Nadhani mnaona jeuri ya pesa aliyoifanya Tanasha. Hana njaa, ameamua kuteketeza pesa na hapo anakwambia hana muda wa kumpeleka mtoto Bongo kwa baba’ke, anapambana kulea mwenyewe.

“Tanasha siyo kama mama watano (Zari),” aliandika shabiki wa Tanasha kwenye moja ya video za shughuli hiyo kwenye Mtandao wa Instagram.Bila kupepesa, shabiki mmoja wa Zari alijibu kwa kumuita, Tanasha ni Harmonize wa kike!“Hivi unaweza kumtofautisha Tanasha na Harmonize?

Maana tunaona kila kitu anachofanya Diamond, lazima Harmonize aige. Ona sasa kwa bishosti (Tanasha) amekopi hadi jina la All White Party…” aliandika shabiki huyo ambaye ni Team Zari.Tanasha amejaaliwa mtoto mmoja wa kiume na Mondi aitwaye Naseeb Junior huku Zari akijaaliwa wawili na jamaa huyo. Tiffah Dangote na Prince Nillan.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR

Leave a Comment