×

Magufuli Aongoza Baraza la Mawaziri, Mwinyi Aapishwa – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma leo Desemba 16, 2020.

Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumatano Desemba 16, 2020 anaongoza kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri kinachofanyika mjini Dodoma.

 

Katika kikao hicho Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma akimwapisha Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Tanzania kabla ya Rais John Magufuli kuongoza kikao cha baraza hilo.

Mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu, Gerson Msigwa amesema, “leo tutashuhudia mmoja wa wajumbe wa baraza hili akila kiapo ukumbini hapa na kuwa mjumbe halali wa baraza la mawaziri.”

 

Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan na waziri mkuu, Kassim Majaliwa ni kati ya waliohudhuria kikao hicho pamoja na mawaziri na manaibu waziri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzaniajijini Dodoma leo Desemba 16, 2020.
Rais Magufuli akishuhudia Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akimkabidhi nyenzo za kazi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma leo Desemba 16, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma leo Desemba 16, 2020

Leave a Comment