×

Nyakua Friji, Mashine ya Kufulia, na Smart Tv Kutoka Infinix

Afisa Uhusiano wa Infinix Tanzania, Aisha Karupa (kushoto) alipokuwa akizindua kampenio hiyo.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Infinix imezindua rasmi Kampeni ya Christmas na Mwaka mpya inayofahamika kama HIT THE JACPOT BE A WINNER ikiwa na maana jaribu na ushinde ambapo ukinunua Infinix NOTE 8, ZERO 8 na HOT 10 utakuwa umejiweka katika nafasi ya kujishindia zawadi kemkem kama vile, Infinix NOTE 8 mpya na (Washing Mashine, Friji na Smart TV). Je ni vipi unaweza kujishindia zawadi hizi?

Kupitia Facebook

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Afisa Uhusiano wa Infinix Tanzania, Aisha Karupa amesema ili kushiriki kampeni hiyo, tembelea maduka ya Infinix, nunua simu zilizotajwa hapo juu kisha utapatiwa vifurushi vyenye zawadi za Infinix ikiwemo na kadi ya krismasi, piga picha ukiwa na kadi hiyo pamoja na slot mashine ambayo inapatikana madukani kwetu, post kwenye account yako ya Facebook na #infinix jackpot.

Sehemu ya zawadi hizo pichani.                           

Kupitia Xclub,

Ibuka mshindi kwa kujiunga moja kwa moja kupitia app ya Xclub ambayo ni maalumu kwa watumiaji wa Infinix, chakufanya jiunge na app hiyo kisha unganisha na rafiki zako wawili papohapo na baada ya kujiunga utaingia kwenye Xstore na kuchagua bidhaa uipendayo kama vile Infinix NOTE 8, ZERO 8 au HOT 10 lakini pia utakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kushindania Mashine ya kufulia, Friji na Smart Tv au vyote kwa pamoja.

Kampeni hii itadumu kwa takribani siku 30 kuanzia tarehe 16/12/2020-15/1/2021 ambapo kila wiki Infinix itatangaza washindi ambao wataingia katika droo kubwa itakayochezeshwa tarehe 13/1/2021. Alimaliza kusema Aisha.

Kwa maelezo zaidi tembelea madukaya Infinix vilevile tembelea@infinixmobiletz

Leave a Comment