×

Babu Tale, DC Watua Kwenye Gereza la Mtego wa Simba – Video

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msurwa akiwa ameambatana na Mbunge wa Morogoro Kusini, Babu Tale, wameupongeza uongozi wa Gereza la Mtego wa Simba kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Jengo jipya la kisasa la Mama na Mtoto litakaloanza kutoa huduma hivi karibuni.

 

Ujenzi huo umeanza mara baada ya Jengo la awali kuzidiwa, ambapo kituo hicho kilikuwa kikitoa huduma kwa Wafungwa, Askari pamoja na Familia zao, lakini kwa sasa kituo hicho kimekuwa kikihudumia jamii nzima iliyo izunguka gereza hilo.

 

Mkuu wa Wilaya pamoja na Mbunge wameahidi kuweka nguvu katika Jengo hilo ili liweze kukamilika mapema na kutoa huduma kwa wananchi na waweze kufaidi matunda ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John P. Magufuli.

 

Leave a Comment