×

Breaking: Mama Mzazi Wa MC Pilipili Afariki Dunia -Video

MCHEKESHAJI wa Bongo, MC Pilipili  usiku wa kuamkia leo Desemba 20, 2020 amefiwa na Mama yake mzazi, Mama huyo amefariki sambamba na mdogo wake Mama mdogo wa MC Pilipili baada ya kupata ajali walipokua wanaelekea ukumbini kusherehekea harusi ya mdogo wake Mc Pilipili iliyokua inafanyika Mbezi Beach.

 

MC Garab ambaye ni Mtu wa karibu na MC Pilpili, amethibitisha taarifa hizo na kusema “Hakika ni pigo kubwa kwa Harusi kugeuka msiba mkubwa namna hii, mipango ya mazishi inafanywa, tuiweke familia katika maombi”

 

“Ulale salama Mama yangu Mpenzi Mariam Matebe, umetufundisha upendo na umefariki ukijariibu kuonesha upendo, lala salama Mpenzo RIP” ameandika @mcpilipili #RIPMamazetu🙏🙏

Leave a Comment