
MWANADADA Rachel Said maarufu kama Wema wa Buguruni, mkazi wa Buguruni Rozana, jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita alifunga mtaa baada ya kufanya sherehe yake ya kuzaliwa (bethidei).
Sherehe hiyo iliyofunga mtaa ilijumuisha watu mbalimbali wa kutoka viunga vya Tabata, Ilala, Mbagala na Gongo la Mboto.
Kama unajiuliza kwa nini watu walikuwa wengi, jibu ni rahisi tu, Wema wa Bunguruni ni mtu wa watu, jina lake ni kubwa na linafanana na watu waliofika kwenye ishu yake hiyo.
AUZA VIJORA 300
Ili kuonesha wazi ni jinsi gani anakubalika karibia Buguruni nzima, Wema huyo aliandaa sare yake ya siku yake hiyo ya kuzaliwa ambapo aliuza vijora 300 kwa sababu kila mtu alikuwa anaitaka kuvaa sare hiyo na asikose kuhudhuria kwenye sherehe hiyo iliyofanyika kwenye mtaa anaoishi.
“Nakuambia kuwa nilileta vijora karibia mara tano vikaisha vyote mpaka vimefika mia tatu na hapo bado watu wamekosa kama ulivyoona wananiomba tena na leo ndio siku yenyewe,” alisema Wema huyo wa Buguruni.
MAMA MZAZI CHENI
Kutokana na mapenzi makubwa aliyokuwepo nayo mtoto wake kwa Wema Sepetu (halisi), mama mzazi wa mwanadada huyo aliamua ‘kumsapraizi’ mtoto wake huyo kwa kumchongea cheni ya Sliva yenye thamani ya shilingi 120, 000, yenye jina la Wema Sepetu na kusema kuwa watu wasimshangae sana mwanae kwani mapenzi ya kumpenda mtu yapo.
“Nimemfanyia sapraizi mwanangu kumchongea cheni kwa sababu ana mapenzi makubwa na nawashangaa sana watu ambao wanambeza mtoto wangu kwa sababu si ajabu kumpenda mtu kwa maana na yeye binadamu,” alisema mama huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.
AMTUNZA WEMA SEPETU DIRA
Licha ya kuwa staa huyo wa filamu hajafika kwenye bethidei ya mrembo huyo, mwanadada huyo aliamua kumtunza dera Wema na kuomba limfikie popote alipo kama ishara ya upendo kwake kila siku.
“Nimemtunza dera Wema, naomba limfikie popote alipo nikimuona ndio nitatinga na kigoma kabisa lakini mtaa huu umefurika kwa ajili yake, asikwambie mtu nampenda jamani,” alisema mwanadada huyo ambaye baada ya kusasambua barabarani, walitinga ukumbini kuendelea na sherehe ya kukata na shoka.