×

Shuhudia Maajabu ya Machinjio ya Vingunguti

KUFUATIA maagizo aliyotoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, kwa machinjio ya kisasa Vingunguti kuhakikisha wanarekebisha kasoro zilizoonekana kwenye jaribio la kwanza la uchinjaji ikiwemo kasi ndogo ya uchinjaji, kukosekana kwa elimu ya matumizi ya mitambo, hatimaye jaribio jingine la uchinjaji limeonyesha ufanisi.

Akiongozana na wakuu wa wilaya za mkoa huo, Kunenge aamefika na kujionea vijana wa wakifanya zoezi la kuendesha mitambo hiyo baada ya kupatiwa elimu ya matumizi yake, jambo lililosaidia kuongezeka kwa kasi ya uchinjaji.

Akizungumza baada ya kujionea zoezi hilo amesema kasi ya uchinjaji kwa siku ya jana imeonyesha matokeo mazuri lakini bado yapo mapungufu madogo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho.

Aidha, amewaelekeza wahusika wa mradi huo kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa kwa vijana hao ili waendelee kupata uzoefu wa kutosha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija, amesema machinjio hayo yatatoa ajira kwa vijana zaidi ya 300 na yatakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 1,000, mbuzi 1,000 na kondoo 1,000 kwa siku ambapo zoezi la uchinjaji wa ng’ombe mmoja linachukua takribani dakika 15.

Leave a Comment