
NGULI wa muziki wa dansi aliyewahi kuwa mwanamuziki wa kundi la Chuchu Sound, Mao Santiago, amefariki dunia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mao alihudumu kama mwimbaji katika bendi kadhaa hapa nchini ikiwemo Chuchu Sound, The Stars na Machozi Band.
Mwanamuziki mwenzake wa dansi, Hamisi Mbizo maarufu kama H. Mbizo, amethibitisha kutokea kwa msiba huo.
Kwa taarifa zaidi endelea kuwa karibu na mitandao yetu.