
MSANII wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Hunai Ramadhani ‘Official Nai’ amewachana baadhi ya wasanii wanaotegemea ushirikina kwenye kazi zao.
Akizungumza na AMANI, Nai amesema kuwa kulogana ni ushamba na wanarudisha wenzao nyuma hivyo amewaomba wasanii wenzake waweze kulogana kwa kazi nzuri.“
Naona kuloga siyo ishu nzuri kabisa, kwa wasanii kwa sababu unamrudisha mwenzako nyuma kila mtu anatafuta riziki yake, hivyo basi mimi ningewaomba wasanii wenzangu tulogane kwa kuachia muziki mzuri tu basi huo ndiyo uchawi mkubwa,”alisema Nai ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Siyo Saizi Yao