×

Kaze Apata Kombinesheni ya Ubingwa Yanga

NI wazi sasa Kocha wa Yanga, Cedric Kaze ameipata kombinesheni hatari ya utatu mtakatifu kupitia kwa wachezaji Yacouba Songne, Saido Ntibazonkiza na Deus Kaseke ambao tangu awatumie kwa pamoja wameleta faida kubwa kikosini hapo.

 

Yanga msimu huu wametangaza kulisaka taji la Ligi Kuu Bara mara baada ya kulikosa kwa misimu mitatu, ambapo kwa sasa wao ndio ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 43 Hapo awali Yanga ilikuwa ikipata shida katika sula la kufunga mabao mengi jambo ambalo kwa sasa limepotea kutokana na uwepo wa kombineshi hiyo hatari ya utatu mtakatifu ambayo imefanikiwa kuzalisha mabao sita ndani ya michezo mwili.

 

Katika michezo hiyo miwili, Yanga ilianza kuifunga Dodoma Jiji mabao 3-1 ambapo Kaseke alifanikiwa kutoa asisti, huku Saido akifunga na kutoa asisti.Mchezo wa pili dhidi ya Ihefu, Yanga ilishinda 3-0.

Bao la kwanza lilifungwa na Kaseke akipokea pasi ya Saido, bao la pili la Yanga lilifungwa na Yacouba akipokea pasi ya Ntibazonkiza, huku bao la tatu likifungwa na Feisal Salum ambaye alipewa pasi na Kaseke.

 

Kutokana na ubora wa wachezaji hao, Kaze ameanza kufurahishwa na kombinesheni hiyo ambapo katika michezo yote hiyo miwili ameonekana akiwatumia katika kutafuta mabao.

 

Leo Alhamisi, Yanga watakuwa na kibarua cha kumenyana na Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Leave a Comment