×

TRA Yavunja Rekodi, Yakusanya Tril. 2 Kwa Mwezi – Video

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dr. Edwin Mhede, leo Januari 1,  2021 amesema mamlaka hiyo kwa Desemba 2020 imepata mafanikio ya kukusanya Sh. trilioni 2.088.

“Tulikuwa na lengo la kukusanya fedha taslimu trilioni 2.072 kwa Desemba 2020 lakini tumekusanya trilioni 2.088 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 101 ya lengo hilo.  Makusanyo haya ni ya kihistoria, hatujawahi kukusanya fedha kiasi hicho toka TRA imeanzishwa.

“Tunamshukuru Mungu lakini kwa kiasi kikubwa tunawashukuru walipa kodi, tunawapongeza kwa kutimiza wajibu wenu mtukufu na wa kisheria ambao kwa kweli kupitia uletaji kodi hizo za hiari tumefikia hapo,” amesema katika taarifa ya TRA kwa vyombo vya habari.

 

Leave a Comment