The House of Favourite Newspapers

Imebaki stori kwa wasanii hawa

0

Sister P 1Sister P.

Na Mwandishi Wetu
KWA sasa huwezi kutaja maendeleo ya muziki wa kuchana kwa kina dada bila kumtaja mwanadada Nicki Minaj. Nicki ambaye unaweza kusema ndiye ‘top’ wa muziki wa hip hop kwa sasa ulimwengu amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwafanya wadada nao waingie kwenye muziki huo.

Tangu alipoachia ngoma yake ya kwanza iliyomtoa ya Your Love, hakika Nicki aliweza kuwateka mamilioni ya wadada ambao nao walijikuta wakivutika kwa kiasi kikubwa kurap.

Kibongobongo pia zamani kuanzia mwishoni mwa miaka ya 90 waliibuka wadada kadhaa ambao nao walikuwa wanachana, lakini kwa kuwa muziki wa aina hiyo ulionekana kuimbwa zaidi na wanaume baadhi walionekana kukata tamaa mapema.

Lakini hata hivyo wengine walikatishwa tamaa zaidi baada ya kuona kazi zao hazilipi kama vile ambavyo walikuwa wakitoa fedha kwa ajili ya kutengeneza kazi zao.

Pengine sasa hivi ambao bado wanakomaa na ‘game’ ya hip hop kwa kina dada ni Witness, Chiku Keto na dogo ambaye anakuja kiasi chake anafahamika kama Chemical.

Wafuatao ni baadhi ya kina dada ambao walikuwa wanachana hatari lakini leo hii hawasikikiki kabisa kwenye spika za redio na runinga kwa kifupi ni kama imebaki stori;

Zay B
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 ukizungumzia muziki wa hip hop kwa upande wa kina dada hakika ulikuwa huwezi kuliacha jina la mwanadada huyo ambaye kiuhalisia anaitwa Zainab Lipangile.

Zay B aliwika zaidi na Ngoma ya Gado remix aliyofanya na Juma Nature lakini sasa amebaki stori tu kwani hajatoa wimbo wowote uliofanya vizuri kwa muda mrefu sana na inawezekana asirudi tena na kuwika kama zamani.
Ukiachana na ngoma hiyo, bifu kati yake na Sister P lilizidi kumng’arisha dada huyo na mwenzake kiasi cha kuandaliwa shoo ili kumtafuta mkali zaidi.

Sister P
Anakuja anakuja Sister P! Anakuja anakuja ngangari! Enzi hizo wakati michano ya ada huyu ambaye jina alilopewa na wazazi wake ni Happy Pella ipo kitaani ikichana spika za raia wanaopenda burudani hakika alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukusanya nyomi kwenye shoo zake na hicho kilikuwa kipindi chake cha mavuno.

Sister P aliwika na Ngoma ya Anakuja ambapo alisimama peke yake mwanzo mwisho hivyo alionyesha uwezo mkubwa lakini leo hata ukiomba wimbo wake wowote kwenye redio lazima ‘presenter au hata DJ itabidi aweke kwanza ‘headphone’ chini kisha aanze ‘kusambalua’ makablasha ili aweze kumpata.

Leo hii ni ngumu kusikia ngoma zake kali kama Hey Dj, Achana Nao aliofanya na Ally Choky na nyinginezo kibao! Wadau wamekumis rudi Sister P.

DSC04398Dataz.

Dataz
Mrembo huyu alizaliwa mwaka 1984 huko Mbamba Bay, Nyasa, anaitwa Dataz ambaye jina lake halisi ni Florence Kasela. Wimbo uliomtambulisha uliitwa Mume wa Mtu ambapo alifanya na mwanadada ambaye pia ni muigizaji anaitwa Joan. Ngoma hiyo ilitikisa vibaya na kumtambulisha kama kipaji kingine chenye uwezo wa kuchana.

Sasa hivi Dataz hasikiki tena licha ya kuwa kuna kipindi alikuwa akifanya kazi kwa kushirikiana na kaka yake, Squeezer. Mwaka 2010 kidogo alionekana kama angerudi baada ya kushirikishwa na Steve RnB katika ngoma iliyoitwa Sogea Karibu ambapo alichana vizuri na wimbo ulifanya vizuri.

Baada ya kusikika kwenye kolabo hiyo hakuonekana tena kitaani wala kwenye runinga na redio labda kwa media zenye vipindi vya ‘zilizobamba’ ndo anaweza kusikika kwani alikuwa mkalii.

fullRah P.

Rah P
Fredinah Peyton maarufu kama Rah P, ni dada alikuja ghafla na kutoka na Ngoma ya Hayakuhusu ambayo kwa kweli ilifanya vizuri sana, katika listi ya ngoma kali hii nayo ipo.

Baada ya kutoka kimuziki dada huyo alijichanganya lakini ghafla akapotea moja kwa moja mpaka leo huku akiacha msemo wa ‘hayakuhusu’.

Leave A Reply