×

Mmoja Afariki Gari la RPC Likiteketea kwa Moto

GARI la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita na gari ndogo la abiria aina ya Hiace jana, Januari 11, 2021, yaliwaka moto na kuteketea katika ajali iliyosababishwa na dereva bodaboda aliyekuwa amebeba mafuta ya dizeli.

 

Hata hivyo, Kamanda  Hendry Mwaibambe hakuwemo kwenye gari hiyo na amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  akisema majira ya saa 8.46 mchana katika eneo la Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

 

Katika ajali hiyo, dereva wa bodaboda  amepoteza maisha huku watu 16 wakijeruhiwa ambapo wawili kati yao ni polisi.

 

Akielezea tukio hilo, Mwaibambe amesema dereva wa bodaboda huyo alikuwa amebeba lita 100 za mafuta ya dizeli akaingia barabarani bila umakini na kugongwa na gari ya kamanda kisha kwenda kugonga HMiace iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara na kusababisha magari yote kuwaka moto.

 

Amesema gari hiyo ya polisi yenye namba PT 4447 iliyokuwa ikiendeshwa na Koplo Manase Nestory iliwaka moto kufuatia cheche za pikipiki iliyoangukia mafuta yaliyomwagika.

 

Kwa mujibu wa kamanda hmuyo, majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya ya Chato na kwamba hali ya dereva wa Hiace ni mbaya huku polisi wakitibiwa na kuruhusiwa kuondoka.

 

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment