The House of Favourite Newspapers

Chikwende Anukia Ndani ya Simba

0

IMEELEZWA kuwa Perfect Chikwende nyota wa Klabu ya FC Platinum yupo kwenye hesabu za mwisho kutua ndani ya Klabu ya Simba.

 

Awali nyota huyo ambaye alimtungua Aishi Manula kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika alikuwa anatajwa kutua ndani ya Azam FC.

 

Mabosi wa Azam wanatajwa kuwa walikuwa wanahitaji kumuongeza ndani ya kikosi hicho ila Kocha Mkuu, George Lwandamina inaelezwa kuwa alikuwa hajamuelewa.

 

Taarifa zinaeleza kuwa Chikwende amemalizana na Simba baada ya Lwandamina kuwafanya viongozi wa Azam kupunguza nguvu katika dili hilo na kuwaachia Simba mwanya wa kumnasa winga huyo.

 

Huyo anakuwa nyota wa pili kumalizana na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo baada ya kuanza na Thadeo Lwanga ambaye ni kiungo mkabaji.

 

Lwanga alikuwa kwenye kikosi cha Simba ambacho kimeshiriki Kombe la Mapinduzi na alicheza pia kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga.

Leave A Reply