
MCHUMI wa Benki Kuu ya Rwanda, Thomas Kigabo amefariki dunia leo Januari 15, 2021 kutokana na Covid-19.
Amefariki mjini Nairobi, Kenya, ambako alikuwa akipata matibabu.
Kigabo amekuwa mchumi mkuu katika Benki Kuu ya Rwanda kwa zaidi ya miaka kumi. Alikuwa pia mhadhiri wa chuo kikuu na mhubiri.
Ni ofisa wa ngazi ya juu zaidi wa serikali ya Rwanda kufa kutokana na Covid-19 nchini humo.
Hadi sasa Rwanda imerekodi watu 10,000 waliopatwa na virusi vya corona na vifo 133.
Benki Kuu ya Rwanda imetoa taarifa kuhusu kifo chake kupitia mtandao wa Twitter:
