

WAKATI Kampuni ya Global Publishers Ltd ikizidi kwenda kasi katika ulimwengu wa kidijitali, leo tena timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo wameendelea kutoa elimu juu ya namna wasomaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi na Amani wanavyoyapata kwa njia ya kidijitali ambapo baadhi yao wamesema ujio wa magazeti hayo kwa njia ya mtandaoni imewasaidia kuondoa usumbufu wa kutembea na nakala mkononi.
Maofisa hao wameingia tena mtaani maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa wasomaji wa Magazeti Pendwa kuendelea kujipatia uhondo wa habari za burudani kupitia mtandaoni.

Akizungumza na wasomaji wa maeneo hayo, Mkuu wa kitengo cha masoko, Anthony Adam amesema kuwa Kampuni ya Global Publishers katika kuhakikisha inawajali wasomaji wake na wanaendana na kasi ya ulimwengu wa teknolojia, wameamua kuwawekea magazeti hayo kwa mfumo huo ili kuwarahisishia na kuokoa muda wao ambao walikuwa wakiupoteza kwa kwenda katika meza za wauzaji na hata kukosa kabisa muda wa kuyafatilia.
“Tumeamua kuwarahisishia muyapate Magazeti yetu Pendwa kupitia njia ya mtandao. Hii yote ni kutokana na dunia inavyokimbia kasi katika ulimwengu wa teknolojia ambapo tutaendelea kuwajali kwa kuwapatia habari motomoto kupitia mtandao tena kwa bei ya Tsh 300/= kuanzia mwezi ujao wakati kwa mwezi huu yakipatikana bure mtandaoni,” amesema Adam.

Mmoja wa wasomaji wa Magazeti Pendwa aliyejitambulisha kwa jina la Ester Ayubu mkazi wa Kimara Korogwe ameipongeza Global kwa kuendana na kasi ya teknolojia akisema kuwa uwepo wa magazeti hayo mtandaoni unamsaidia kuokoa muda aliokuwa akiutumia kuyafuatilia katika meza za magazeti na badala yake anatumia simu yake ya mkononi kufanya malipo pale tu wateja wanapopungua na kusoma.
“Global mmetufanyia jambo jema, sasa hivi yaani nikiwa tu hapa kwenye saluni yangu napitia magazeti hayo wateja wakiwa wamepungua na ninapata habari nyingi tu za wasanii tena kwa urahisi kabisa tofauti na mwanzo ambapo gazeti hadi ufatilie. Asanteni sana kwa kuturahisishia,” alisema.

Kwa msomaji, ili kuyasoma magazeti hayo ni ku-downlo adapplication yako ya Global Publishers ili usome hadithi uzipendazo za Eric Shigongo na habari za magazeti ya Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi na Amani, BURE kwa mwezi mzima hivi sasa sasa!
Baada ya OFA hii, utayasoma kwa bei rahisi ya shilingi 300 tu kwa nakala popote ulipo, ndani na nje ya Tanzania, kupitia Global App au website ya www.globalapp.co.tz#GlobalApp #GlobalPublishers #Uwazi #Risasi #Amani #IjumaaWikienda.