×

Mrithi wa Mkude Athibitisha Kumalizana na Simba

NI rasmi sasa kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya DR Congo, Doxa Gikanji amethibitisha kumalizana na uongozi wa Simba juu ya kujiunga na timu hiyo huku akisema kuwa kuna asilimia kubwa ya yeye kujiunga na Simba mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) ambayo bado inaendelea kufanyika nchini Cameroon.

 

Gikanji, 30, anakipiga katika Klabu ya DC Motema Pembe inayoshiriki Ligi Kuu ya DR Congo na kwa sasa mchezaji huyo yupo katika kambi ya timu hiyo ya taifa nchini Cameroon.

⚫️ Kwa UPDATES za Michezo, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja kutoka Cameroon,Gikanji alisema ni kweli yupo katika mazungumzo na Simba ambayo yamefikia sehemu nzuri na kama yataendelea kuwa hivyo basi atalazimika kujiunga Simba mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya CHAN.

“Nimefanya mazungumzo na Simba juu ya wao kunihitaji, tayari tupo katika mazungumzo ambayo kwa kiasi kikubwa yamefika pazuri, kama tufanikiwa kwa pande zote mbili basi mara baada ya kumalizika kwa michuano ya CHAN basi itanibidi nije Tanzania moja kwa moja kujiunga na Simba,” alisema kiungo huyo.

 

⚫️ Kwa UPDATES za Michezo, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

Aidha, usajili wa kiungo huyo ndani ya Simba ni ishara tosha kuwa viongozi wa timu hiyo hawajaridhishwa na kiwango cha kiungo mkabaji Thadeo Lwanga ambaye inasemekana huenda akaachwa mara baada ya kuwasili kwa kiungo huyo, pia ikiwa ni ishara kuwa Jonas Mkude anatakiwa kujipanga kwa kuwa wanacheza nafasi moja.Walipotafutwa viongozi wa Simba kuhusu suala hilo, hawakuonyesha mwitikio wowote hadi tunaingia mitamboni.

MKUDE AOMBA RADHI

Aidha, Jonas Mkude, jana jioni aliamua kutumia ukurasa wake wa Instagram kuomba radhi Wanasimba wote kwa kilichoelezwa kuonyesha utovu wa nidhamu na kufikia hatua ya kusimamishwa kazi.

 

⚫️ Kwa UPDATES za Michezo, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

“Najitwa Jonas Mkude, napenda kuomba radhi kwa Wanasimba wote, tumeumbwa kukosea lakini haimaanishi nitakosea tena.“Mimi ni mwanasimba mwenzenu na klabu hii ni sehemu ya maisha yangu!“Naamini wachezaji wenzangu, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na washabiki mtanielewa na mtanisamehe,” alisema Mkude.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

DIAMOND AKIWA na MTOTO wa TANASHA NYUMBANI KWAKE Baada ya KUTUA BONGO..

Leave a Comment