×

JPM Azindua Jengo la Wagonjwa Kahama – Video

RAIS John Magufuli ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 28, 2021 na kuwataka wafanyakazi katika hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii.

 

 

Akiwa katika jengo hilo, Magufuli aliyeambatana na Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo,  amesema serikali inaendelea kushughulikia kero za afya ikiwa pamoja na kuajiri watumishi wa sekta hiyo.

 

 

“Katika miaka mitano tumetoa ajira za watumishi wa afya zaidi ya 14,000 na tuliajiri madaktari 1000 mwaka jana. Ninafahamu katika miaka mitano iliyopita, madaktari na wauguzi hamkuniangusha.

 

 

“Changamoto za huduma za afya ninazifahamu tutaendelea kuziboresha ili na nyinyi mwendelee kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa,” amesema.

 

 

Baada ya kauli hiyo, kiongozi mkuu huyo wa nchi alitoa Sh mil. 1 na kuwapatia watumishi hao kabla ya kukagua moja ya wodi za hospitali hiyo na kuwasalimia wagonjwa.

 

 

Jengo hilo lililofikia asilimia 65 ya ujenzi wake lina maeneo 62 ya kutolea huduma za macho, meno, huduma ndogondogo, chumba cha upasuaji na ofisi za utawala.

 

 

Leave a Comment